Zaidi ya mashirika 2,000 na wawakilishi kutoka mbalimbali zikiwemo nchi za Uganda, Ethiopia, Zambia na Malawi wanatarajiwa kushiriki Jukwaa la nne la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO huku Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko, akitarajiwa kulifungua rasmi.
Hayo ameyabainisha leo Jumatatu Agosti 26, 2024 Mwenyekiti wa NaCoNGO, Jasper Makalla jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu jukwaa hilo na kusisitiza litahusisha kubadilishana uzoefu, kushirikishana changamoto na kutoa suluhisho, ili kuboresha mazingira wezeshi kwa NGO’s nchini.
Jukwaa hilo litaandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu na Ofisi ya Msajili wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini.