Zaidi ya shilingi milioni 200 zinatarajiwa kukusanywa na kufanikisha ujenzi wa ukuta wa shule ya sekondari ya wasichana ya Songea kufuatia michango ya wanafunzi waliowahi kusoma miaka ya nyuma .
Ujenzi huo ambao ni msaada wa wanafunzi ambao walisoma katika shule ya sekondari ya wasichana ya Songea miaka ya nyuma unatizama kama mchango wa kukuza na kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi wa wanaosoma kwa sasa katika shule hiyo iliyopo manispaa ya Songea.
Afisa elimu wa sekondari kutoka Halmashauri Manispaa ya Songea Bi, Janeth Moyo amesema ” Hii kwetu ni jambo kubwa sana kwani hawa wameamua
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya wasichana ya Songea Esther Kolomola amesema ” kujenga kwa ukuta huo kutakwenda sanjari na maboresho mengine huku akiwaomba wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kuendelea kuchangia shule hiyo ili iendelee kuwa kitovu cha maarifa kwa wasichana wa sasa.
Naye mmoja wa wachangiaji ambaye aliwahi kusoma shule hiyo ya Wasichana ya Songea Cecilia Mtawa amesema uamuzi wa kujitolea michango hiyo ni kukumbuka fadhila na kutoa heshima kwa shule hiyo iliyo wasaidia wengi kupata maarifa kwa miaka ya nyuma.