Top Stories

Zaidi ya Watumishi wa Afya 9,000 wapata Corona Hispania

on

Idadi ya Watumishi wa idara ya afya walioambukizwa Virusi vya Corona nchini Uhispania imefikia 65,719 na imeelezwa kuwa 9,444 kati yao ni watumishi wa Sekta ya Afya.

Wizara ya Afya imesema Uhispania ina idadi kubwa zaidi ya watumishi wa afya walioapata maambukizi ya COVID19 duniani. Idadi ya vifo iliyoripotiwa hadi sasa nchini humo ni 5,138 na waliopona ni 9,357.

Kufuatia uhaba wa vifaa vya kujikinga na maambukizi duniani kote, Serikali imesema ipo vitani kupata mashine za kupumulia, barakoa (face mask) na vipimo kwasababu kila nchi inapigania kupata vifaa hivyo.

TIMBWILI LAIBUKA, MAKONDA WAMVAA AFISA ALIETAKA KUWAPORA LESENI KISA KUJAZA ABIRIA

Soma na hizi

Tupia Comments