Taarifa inasema boti ya Kilimanjaro II iliyokua ikitokea Pemba kwenda Unguja January 5 2014 sehemu yake ya mbele ilizama kwa dakika kadhaa kwenye mkondo wa maji ndani ya eneo hatari la Nungwi ambapo watu kadhaa waliokua wamekaa sehemu hii ya mbele kwenye picha inayofata hapa chini walibaki kwenye maji baada ya dhoruba hii.
Baada ya hapo inadaiwa ilibidi watu hao waachwe bila kuokolewa badala yake wakatupiwa vifaa vya kujiokoa na safari ikaendelea ili kuepusha boti nzima isizame.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia millardayo.com jana usiku (Jan 5 2013) zilisema katibu wa makamu wa pili wa Rais Znz akifanya mahojiano na Zanzibar cable TV alithibitisha kupatikana kwa maiti 5 na majeruhi watatu wakiwa taabani kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Unataka kuwa karibu na matukio mbalimbali yanayotokea nje na ndani ya Tanzania? ungana na kuwa mwanafamilia kwenye facebook, twitter na instagram zenye jina la Millard Ayo na utakua ukitumiwa taarifa kila zinapotokea.
Huyu ni miongoni mwa waliookolewa.
Hapa kwenye hii picha juu ni baada ya boti kuzama kwa sehemu ya mbele na kuibuka tena, ilipoendelea na safari abiria wote wakaamua kuvaa vifaa vya kujiokoa.
Kwenye picha ya juu na chini ni jinsi viti vilivyongo’lewa na maji yenye nguvu wakati sehemu hii ya mbele ilipozama kwa dakika kadhaa ambapo shuhuda Hamis alisema baada ya kuzama boti ilizima kwa dakika kama tano mpaka ikaanza kusogezwa na maji na kisha baadae ikakubali kuwaka ndio wakaendelea na safari.