Shirikisho la soka Duniani (FIFA) limeiandikia barua chama cha soka Misri (EFA) na kueleza kuwa wameifungia club ya Zamalek kufanya usajili hadi wailipe Sporting CP hela zao za usajili za mchezaji Mahmoud Shikabala.
Shikabala alijiunga na Sporting 2014 akitokea Zamalek kwa euro 190,000 (Tsh milioni 510) na aliondoka 2015 kurejea Zamalek kwa euro 570,000 (Tsh Bilioni 1.5) baada ya kucheza mechi moja tu katika miezi 18 aliyokaa Sporting.
Inaaminika sasa deni la Sporting kwa Zamalek kwa sasa linafikia USD milioni 1.5 (Tsh Bilioni 3.6), hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa Zamalek kufungiwa kufanya usajili kwani waliwahi kufungiwa madirisha mawili msimu wa 2021/22 kutokana na kuwa na kesi na mchezaji Hossam Ashraf na Kocha wao wa zaman Christian Gross.
Tazama pia;