Habari za Mastaa

Zamaradi afunguka baada ya kumuweka mumewe kwenye bango (video+)

on

Mtangazaji/Mjasiriamali Zamaradi ameingia kwenye trend mitandaoni baada ya kutundika barabarani bango lenye picha ya Mume wake.

Baada ya kusambaa kwa picha hii Ayo TV ilimpigia simu Zamaradi ili kufahamu mengine ambapo amesema bango hili ambalo alianza kuliandaa kwa wiki mbili zilizopita bila Mume wake kufahamu, limewekwa jana February 13 saa kumi na mbili jioni na amelilipia litakaa hapo kwa muda wa mwezi mzima “hii ni barabara ambayo anapenda sana kupita yani kila siku lazima apite ndio maana nimeliweka pale”

“Baada ya kuliweka nilimchukua mpaka pale amefurahi sana, tulipofika pale alicheka sana alafu akaingia kwenye gari machozi yakawa yanamtoka akaanza kulia akawa ameinama kwenye gari akasema kwahiyo Mke wangu umeamua kuniweka hapa juu…… amefurahi sana kwakweli”

“Sasa hivi tuna miaka mitano ya ndoa lakini sita ya mahusiano, nia yangu kumuweka kwenye bango ni jinsi ninavyompenda, ninampenda sana Mume wangu, Mume wangu amekua ni Mtu flani ambae amenifanyia vitu vingi hakuna Mtu ambaye anaweza akajua”

Unaweza ukabonyeza play kujionea Zamaradi alivyomuweka mumewe kwenye bango.

 

Soma na hizi

Tupia Comments