Top Stories

“Zanzibar itakuwa kitovu cha uchumi barani Afrika” Maalim Seif

on

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi barani Afrika.

Maalim ameyaeleza hayo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Alabama Michenzani Wilaya ya Mjini Unguja.

Maalim Seif amesema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa na bandari, ambayo wafanyabiashara wataweza kuingiza bidhaa zao bila ya ushuru na wakati wa kutoa watatozwa ushuru kidogo sana.

Amesema akilifanya hilo, wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki na Kati wataweza kuingia Zanzibar na kujipatia bidhaa zote wanazozitaka na ushuru utakuwa mdogo.

Maalim Seif kadhalika aliweka wazi kuwa katika miaka yake mitano atahakikisha Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ambalo ndege zake zitatembea duniani kote.

LIVE: MAELFU YA WATU WAKIWAPOKEA MAALIM SEIF, MEMBE, ZITTO KABWE ZANZIBAR

Soma na hizi

Tupia Comments