Zarina Hassan ( Zari ) ambaye ni Mama Watoto wa Mwimbaji Diamond Platnumz, amewasili Tanzania usiku wa kuamkia leo March 21,2024 na asubuhi hii ameongea na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ukaribu wake na Msanii Zuchu ambaye amesema ni Mtu mzuri na hata Watoto wake wakiwa Tanzania huwa kwenye mikono salama na huwa anawasiliana na Zuchu kujua maendeleo yao.
Zari amesama hayo wakati aksign mkataba mwingine na Kampuni ambayo amekuwa akifanya nayo kazi kwa zaidi ya miaka mitatu ya Softcare huku akiwa analipwa fedha nyingi na kusema “Nimekuwa nikifanya kazi vizuri na kampuni hii ndiomana wamefurahia kuongeza mkataba na mimi ambaye brand yangu imezidi kuwa kubwa east afrika yote na brand hii ipo mpaka Ghana”
Na kuhusu swala la Diamond na wazazi wenza Zari amesema “Watu wanachukuliaga eti Mimi siongei na Wanawake wa Diamond, naongea na Zuchu hata kama Watoto wanakuja Tanzania simtafuti hata Baba T (Baba Diamond) hata kumwambia eeh jamani kinachojiri, nampigia Zuchu namwambia hey za asubuhi mnaendeleaje atajibu aah tunafanya hivi tunaenda swimming, kwasababu sioni tatizo kwanza Zuchu Mtu mzuri sana na Watoto wangu wakiwa huku wanakuwa na utulivu kabisa kuwa na yeye”
“Kuhusu Mtoto wa Hamisa Diamond mwenyewe atajielezea kama Mtoto wake ama sio wake Mimi sijui, akiniambia huyu ni Mtoto wangu nataka ajuane na hawa wangu nitamkaribisha”