Mix

Habari mbili kubwa zilizoruka kwenye Televisheni Usiku wa leo June 22, 2017

on

Leo June 22, 2017 pamoja na story nyingi ambazo zimeripotiwa na Televisheni mbalimbali za Tanzania nimekusogezea hizi mbili kubwa zilizosomwa kwenye Taarifa ya Habari ya Channel Ten…

Oparation ya TRA, Yafunga maduka ya wafanya biashara Kariakoo DSM

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imeendesha oparationi ya kuwafungia wafanyabiashara wa Kariakoo DSM ambao wameshindwa kutii maagizo ya kufika ofisini kwao pindi wanapokutwa na makosa mbalimbali ikiwemo kutokutoa risiti kwa wateja na wasio na mashine za kieletronic za EFD.

Maafisa hao wa TRA wamefika katika maduka kadhaa ambayo kwa asilimia kubwa yamekutwa na kosa la kutokutoa risiti baada ya kufanya mauzo ambapo watatozwa faini ya kuanzia shilingi Milioni Tatu hadi Nne na nusu kulingana na mazingira. 

“Yaani kero yetu sisi wanaokuja kutukamata kwa ajili ya mashine sisi kule ndani tunakaa kama Machinga na pale mezani mzigo wangu haufikii hata wa huyo Machinga wa njee ila wanakuambia ukishaingia ndani ya fremu unatakiwa kulipa kodi na utumie mashine.

“Mimi msingi wangu Laki Tano na hiyo mashine Laki Saba, mimi nitanunuaje? Bora hata ingekuwa inatolewa bure useme nitatumia kwa kuwa inatolewa bure.” – Abela Rafael.

Sakata la Kipindupindu lamng’oa Kaimu Mganga Mkuu, Nkasi Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Mgangan Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Dkt. Makundi Mazige kwa kosa la kushindwa kutoa taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu ambapo zaidi ya watu 90 wameugua kipindupindu na mmoja kupoteza maisha katika wilaya yake tangu May 14, 2017.

“Wilaya imekuwa ikishughulikia hili jambo kwa siri tena siri kubwa sana kwa sababu zilikuwepo dalili zinazosemekana kwamba hii ni kipindupindu lakini wao wakafunika kabisa kuwa hakuna tatizo lolote.

“Mganga Mkuu wa Halamashauri ya Nkasi hana namna ya kukwepa jambo hili. Maagazio yangu ni kwamba, kwa kuwa ni maswala yaliyoleta madhara makubwa sana ni vyema akae pembeni na itaundwa Kamati ambayo itakuwa na wataalamu kuona namna gani na hatua zipi zichukuliwe.” – Zelote Stephen

“Hakuna mwenye mimba atakayerudi shuleni” – Rais Magufuli

Soma na hizi

Tupia Comments