Mix

Taarifa ya Polisi Kuhusu milipuko iliyotokea Zanzibar.

By

on

zanjiFebruary 24 2014 kupitia vyombo mbalimbali vya habari stori imesambaa kuhusu milipuko kwenye visiwa vya Zanzibar ikiwa ni milipuko iliyoanza Jumapili ya February 23 2014 na kuendelea mpaka kesho yake.

Polisi kutoka Zanzibar wamethibitisha kutokea kwa milipuko hiyo mitatu ya mabomu kati ya Jumapili na Jumatatu leo mchana visiwani humo ambapo mkuu wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame amethibitisha kutokea kwa milipuko miwili leo February 24 2014.

Milipuko ya leo imetokea katika eneo la mgahawa wa Mercury huku mlipuko mwingine ukiwa umetokea katika eneo la Mkunazini pamoja na mlipuko uliotokea jana Jumapili katika eneo la Pangawe.

Taarifa ya Polisi Zanzibar inasema hakuna vifo wala majeruhi katika matukio yote matatu na pia hakuna mali iliyoharibiwa lakini kutokana na hofu na taharuki ya matukio hayo, kuna madhara ya kisaikolojia yametokea.

Upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika matukio hayo ingawa hadi sasa hakuna mtu au kikundi chochote kilichokamatwa kuhusiana na matukio haya.

Kwa sasa Polisi wanaendelea kuimarisha ulinzi katika sehemu mbalimbali Zanzibar ikiwa ni pamoja na kufanya doria katika maeneo kadhaa huku jeshi hili pia likiwaondoa hofu Wananchi.

Tupia Comments