Habari za Mastaa

Diamond kampeleka Zari Mombasa na kuandika haya maneno 68

on

Ni siku chache zimepita toka Zari ambae ni Mama watoto wa Mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz afiwe na Mama yake mzazi nyumbani kwao Uganda, msiba ambao umetokea mwezi mmoja baada ya Zari kufiwa na Baba watoto wake aitwae Ivan.

Mitandaoni kumekua na maneno mengi ya mashabiki wakisema Zari hajaonekana kama ana huzuni kwenye misiba na kwamba hajawa na majonzi kama kweli kafiwa na Mama yake.

Wakati hayo yakisemwa, Diamond amemchukua Zari na kumpeleka Mombasa Kenya kwa mapumziko na kumliwaza baada ya kupata misiba hiyo ambapo D aliwatolea makavu wanaojifanya wana uchungu wa misiba ya watu.

Diamond alisema kuna watu wanajifanya wanajua sana uchungu wa msiba ya watu “Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo anatakiwa apelekwe sehemu tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja! sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo msijifanye ni tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie”

“Eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia.. pambaneni na mahusiano yenu, nina siku 5 za kumpetipeti leo ndio kwanza ya kwanza”

ULIPITWA? Tazama hapa chini Diamond Platnumz msibani kwa Mama Zari Uganda, afunguka kuhusu zile video za Zari alivyocheza na nduguze wakati Mama mgonjwa

VIDEO: Pesa Zari aliyoitoa kumtibu Mama yake mzazi, PLAY HAPA CHINI

EXCLUSIVE: Zari afunguka baada ya msiba wa Ivan The Don, play hapa chini kupata kila alichosema

Soma na hizi

Tupia Comments