Michezo

Naibu waziri Juma Aweso ametangaza uzinduzi wa Aweso Cup 2019

on

Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Pangani Juma Aweso kesho Jumapili ya April 28 2019, atazindua rasmi michuano ya Kombe la Mbunge wa Pangani linalojulikana kama Aweso Cup 2019, Mbunge huyo ameweka wazi kuendelea na dhamira yake hiyo baada ya kuona matokeo.

Kwa Mujibu wa Naibu Waziri Aweso amesema kuwa kupitia michuano hiyo imetoa vijana wengi msimu uliopita, kiasi cha kuwapelekea kupata timu mbalimbali za mkoa wa Tanga na hata Simba B, hivyo michuano ya mwaka huu imelenga kuzalisha wakina Samatta wengine Pangani.

Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Tsh Milioni 1, mshindi wa pili Tsh laki 6 na uzinduzi wa michuano hiyo utahudhuriwa na watu mbalimbali kama msanii Madee, Steve Nyerere, Haji Manara, DC Jerry Muro huku mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela akiwa mgeni rasmi.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments