Mix

Yaliyonifikia hii leo kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar

on

Ni takribani masaa kadhaa yamebaki ili wananchi wa Zanzibar wafanye maamuzi ya kumchagua Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.

Leo March 19 2016 Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ‘ZEC’ imetoa taarifa kuhusiana na Uchaguzi huo. Taarifa hiyo imetaja waangalizi wa Kimataifa ambao ni kutoka Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Umoja wa Tume za Uchaguzi za Nchi za Kusini mwa Afrika ‘ECF-SADC’, Commoro na Ubalozi wa Zambia ambao tayari wamewasili Zanzibar.

Aidha kupitia taarifa hiyo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar imewaomba wananchi wote kuzingatia ipasavyo maelekezo ambayo yametolewa na yatakayotolewa na Tume katika vituo vya kupigia kura.

Taarifa hiyo pia imesisitiza kuhusiana na upokeaji wa matokeo kwamba wagombea na wafuasi wa wagombea na vyama vyao kuwa tayari kwa matokeo ya ama kushinda au kushindwa. Na pale ambapo mgombea hakuridhika na matokeo ni vyema akatumia njia au taratibu za kisheria katika kutoa malalamiko yake.

Unataka kutumiwa za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana naMillardAyo kwenyeTwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments