Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushinikiza Urusi kufanya amani na Kyiv. Huku akishutumu Iran na Korea Kaskazini kama “washiriki” katika vita vinavyoendeshwa nchini mwake.
Wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likiangazia Mashariki ya Kati, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye aliwasili Marekani siku ya Jumapili Septemba 22, anataka kuweka tahadhari ya kimataifa kuhusu hatima ya nchi yake iliyoharibiwa na vita tangu miaka miwili na nusu.
“Urusi inaweza tu kushinikizwa kuingia katika amani, na hilo ndilo hasa lazima lifanyike: kuishinikiza Urusi kuingia katika amani,” amesema.
Rais wa Ukraine atawasilisha siku ya Alhamisi kwa mwenzake wa Marekani Joe Biden na kwa Bunge la Congress huko Washington maelezo ya “mpango wake wa ushindi” unaolenga kukomesha mashambulio ya Urusi