Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la UVCCM Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Mohammed Ali Kawaida tarehs 22 Februari 2024 wemeanz ziara ya kikazi rasmi Wilaya ya Moshi Mjini Mkoa wa Kilimanjaro.
Katika Ziara hio wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji walitembea na kukagua Miradi mbalimbali ya Vijana Wilayani hapo kuwasikiliza Changamoto zao na kuzifanyia ufumbuzi.
Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni Mradiwa vijana wa Quality Printing Press unaotokana na mikopo ya Halmashauri ya 4% kwa vijana ambapo walipata Tsh. 18,000,000/= na mpaka sasa wamerudisha zote. na kuongeza mtaji wao kufiki zaidi ya Tsh. 100,000,000/=
Kwa niaba ya wajumbe wa Kamati ya utekelezaji Ndg Debora Joseph aliwapongeza vijana kwa kuja na wazo la kujikwamua kiuchumi, amewasihi vijana wa kitanzania kuwaiga vijana hao ili waweza kujipatia kipato pia amewaomba viongozi wa serikali wa wilaya kuwapa ushirikiano vijana hao katika kupata soko na fedha zingine kwaajili ya kuongeza mtaji.
Pia Ndugu Kawaida aliwaongoza wjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza kuu la UVCCM kutembslea shule ya ufundi ya Moshi na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi amewapongeza wanafunzi kuchagua kusoma shule ya ufundi ambapo kwa sasa serikali imeelekeza nguvu kwenye vyuo vya ufundi nchini.
Pia amewasihi wasome kwa bidii lakini wasisahau kufanya mazoezi kwani mazoezi ni Afya, hivyo amewahamasisha kwa kufadhili bonanza la Michozo kwa kutoa 1,500,000/= pamoja na jezi dazen mbili na mipira miwili ya mchezo wa mpira wa Miguu ili wanafunzi waendelee kusoma huku wakiimarisha Afya kupitia michezo.