Duniani

Pesa ya China inaruhusiwa kutumika Zimbabwe? Kilichonifikia ni hiki..

on

Kwa kipindi kirefu Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe hajawa kwenye uhusiano mzuri na nchi za Ulaya na Marekani… upande wa pili Rais huyo amekuwa rafiki mkubwa sana na nchi ya China, na ndiko misaada mingi inakotokea kuingia Zimbabwe.

Mugabe-in-China-600x360

Rais wa China, Xi Jinping na Rais Mugabe

Vichwa vya habari za kimataifa kwenye mitandao mikubwa vimeandika kwamba huenda Zimbabwe wakahalalisha pesa ya China ianze kutumika Zimbabwe kama vile ambavyo pesa yao ya ‘Zimbabwean Dollar‘ inatumika kwenye mzunguko wa kila siku !!

Tuliwahi kusikia mara kadhaa Wabunge wa TZ wakilalamika na kuitaka Serikali kuzuia matumizi ya dola kwenye manunuzi ya bidhaa ndani ya nchi, lakini kwa Zimbabwe mipango ndio iko hivyo.

Rais Mugabe

Rais Mugabe

Zimbabwe imesamehewa deni la dola milioni 40 (hiyo ni zaidi ya Bilioni 80 za Kitanzania) kutokana na msamaha huo, Waziri mmoja Patrick Chinamasa amesema huenda wakapitisha utaratibu wa pesa ya China ambayo ni Yuan ikaingia kwenye mzunguko wa pesa za nchi hiyo na kutumika kwenye matumizi ya kawaida kama njia ya kuboresha uhusiano mzuri wa kibiashara kati ya Zimbabwe na China.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments