Top Stories

Zimbambwe yatangaza maombi siku tatu kisa corona

on

Nchi ya Zimbabwe imeingia katika mfungo wa maombi ya siku tatu kuanzia ili  kujinusuru na  janga la Corona linalowatafuna.

Maombi hayo ya siku tatu yanaongozwa na mke wa Rais wa nchi hiyo Auxillia Mnangagwa na yatamalizika kesho kutwa Jumamosi  kwa maombi ya kushukuru ili kuepukana na janga hilo.

Mke huyo wa Rais  Emmerson Mnangagwa amewaomba wanawake wote wa Zimbabwe na walio nje ya Zimbabwe kuungana nae katika maombi hayo akisema “Tunahitaji kufanya mkakati madhubuti kuanzia nyumbani, kunawa mikono, kuvaa barakoa sahihi cha msingi zaidi kila mmoja azingatie kanuni za afya na kuwa salama kwa kuepuka misongamano.”

Takwimu za  nchi hiyo zinaonyesha kuwa jumla ya watu waliombukizwa virusi vya Corona ni 29,408, watu 879 wakifariki na watu  19,253 wakipona.

MSAKO USIKU WA MANANE, SABAYA AVAMIA GODOWN HEWA AKUTA MAGENDO, PESA, MAFUTA NA POMBE

Soma na hizi

Tupia Comments