Naibu waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Dotto Mashaka Biteko amewataka maofisa na wakaguzi wasaidizi wa Polisi waliohitimu mafunzo yao katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA kuwa waadilifu kama ilivyo misingi ya Jeshi hilo huku akiwataka kuikataa rushwa ambayo inawanyima haki wanao litegemea Jeshi hilo