Top Stories

Zitto “Chanjo ya corona ni salama, kachanjeni”

on

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amepongeza Serikali kuruhusu chanjo, ili Watanzania wapate kinga dhidi ya ugonjwa wa Covid 19, huku akiwahakikishia wanachama wa chama hicho kuwa zipo salama.

Zitto ameeleza hayo leo Jumapili Agosti 8,2021 katika hotuba yake kwa Taifa wakati wa ufunguzi wa kikao cha kamati kuu kinachoendelea Mjini Unguja.

“Napenda kuwahakikishia nimejiridhisha chanjo zilizoruhusiwa kuingia nchini ni salama na mimi nimeshachanjwa, niko salama. Nipende kuwaasa kuwa kuchanjwa ni suala la hiari, lakini tunapoangalia usalama wa wapendwa wetu, jamii yetu na Watanzania wenzetu, hatuna budi kufanya uamuzi sahihi,”  Zitto.

Licha ya kupongeza uamuzi huo, kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwenye uhamasishaji wa watu kujitokeza kupata chanjo.

MESSI ASHINDWA JIZUIA AMWAGA MACHOZI MBELE YA WACHEZAJI WENZIE

Soma na hizi

Tupia Comments