Top Stories

Zitto Kabwe na Mbunge Bwege wakamatwa

on

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amekamatwa leo Juni 23, 2020, na Jeshi la Polisi wakati akiwa kwenye kikao cha ndani cha kupokea Madiwani 8 waliojiunga na chama hicho wakitokea chama cha Wananchi CUF katika Jimbo la Kilwa Kusini.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu “Ndugu Zitto alikuwa Kilwa Kusini kwenye ziara ya kupokea madiwani 8 wa CUF, ambao wamejiunga na chama chetu na leo walikuwa wanakabidhiwa kadi, Polisi wamevamia na wameondoka naye pamoja na Mbunge Bwege na viongozi kadhaa wa Kitaifa, hivyo jumla ni 7, wapo kituo cha Polisi Kilwa tunaendelea kufuatilia sababu na kwanini jambo hilo limetokea” .

ALIYEKUWA MEYA BORA TANZANIA AMUANDIKIA BARUA MAGUFULI “NAITUMA KWA NDEGE” ITAPITIWA

Soma na hizi

Tupia Comments