Mix

Zitto Kabwe kuhusu uchaguzi wa ubunge wa EALA kundi la vyama vya upinzani.

on

Moja ya habari iliyochukua headlines kwenye magazeti ya leo ni pamoja na kuhusu Zitto Kabwe na CHADEMA kudaiwa kutifuana sababu ikiwa ni uchaguzi wa  ubunge wa Afrika Mashariki ‘EALA’. Aidha mijadala mikali imeendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uchaguzi huo kundi la vyama vya Upinzani.

Sasa kupitia ukurasa wake wa Facebook Kiongozi wa ACT Wazalendo ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameyaandika haya…..

ACT Wazalendo kama chama chenye uwakilishi Bungeni kina haki ya kuweka wagombea na tumeshamteua Prof. Kitila Mkumbo katika nafasi 1 kati ya nafasi 3 za Vyama vya Upinzani.

Ninaamini kuwa nafasi 1 hii kuchukuliwa na Mtanzania wa kaliba ya Prof. Kitila Mkumbo haiwezi kuwa ndio hatma ya Upinzani nchini. Eti nafasi moja EALA inayoombwa na ACT Wazalendo kati ya nafasi 3 zilizopo iwe chanzo cha kuvunja Umoja wetu kwenye masuala makubwa ya nchi? We have a war to fight, EALA is just one of the battles. Haiwezi kuwa ndio hatma ya vita kubwa.

Mzee Edward Lowasa hupenda kutumia msemo wa Rais Mstaafu Ahmed Ben Bella wa Algeria ” we have to die a little “. Hekima Hii ni kubwa Sana. ACT Wazalendo kupata kiti kimoja EALA kuwakilisha nchi yetu, tena Kwa kupeleka Mtanzania mmoja bora kabisa hauwezi kuwa kikwazo cha Vyama vya Upinzani kufanya kazi pamoja kwenye mambo makubwa zaidi. Kutaka kuzuia ACT Wazalendo kuweka wagombea wa EALA ni kiwango cha juu cha ukiukwaji wa misingi ya Demokrasia.

Tuweke maslahi ya Nchi mbele Kwa kupeleka EALA watu wenye uwezo mkubwa na wasio na mashaka kuhusu uzalendo wao. Kule EALA tunakwenda kupambana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini. Tukiendekeza vyama na kupeleka watu Kwa sababu ya Vyama vyao tu hatuindei haki nchi yetu. Tuache masihara kwenye maslahi ya nchi.

Tunataka mtu ambaye kwenye Tanzania atasema ” Right or Wrong, my country First “. Prof. Kitila Mkumbo ni mtu wa namna hiyo. Akose kuwakilisha nchi Kwa sababu yeye ni ACT Wazalendo? Kosa lake ni kuwa ACT Wazalendo? Kweli?

VIDEO: ‘Kauli hii kwangu mimi ni ishara ya kufilisika kiitikadi’-Zitto Kabwe, Bonyeza play hapa chini kuitazama

Tupia Comments