Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Maoni ya Zitto baada ya Kenya kuzuia gesi kutoka Tanzania kuingia kwao
Share
Notification Show More
Latest News
Madiwani (3) Waandamanaji 87,wakamatwa nchini Afika ya kusini.
March 20, 2023
Jela kwa mauaji,kuchomoa moyo na kuupika kulisha familia yake “Ninawaondolea mapepo” .
March 20, 2023
Tunisia yaadhimisha Miaka 67 ya Uhuru.
March 20, 2023
Serikali ya Taliban yapiga marufuku zao la bangi.
March 20, 2023
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 20, 2023
March 20, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Mix > Maoni ya Zitto baada ya Kenya kuzuia gesi kutoka Tanzania kuingia kwao
Mix

Maoni ya Zitto baada ya Kenya kuzuia gesi kutoka Tanzania kuingia kwao

April 26, 2017
Share
3 Min Read
SHARE

April 24 2017 iliripotiwa taarifa iliyodai kuwa Wizara ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania kuingia nchini humo ndani ya siku 7, taarifa hiyo ilidai kuwa nia ya Serikali ya Kenya ni kuondoa vituo vya kujaza gesi ambavyo sio rasmi ambavyo vimeibuka katika maeneo mbalimbali ya nchi ambayo vinahatarisha usalama.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ni mmoja wa viongozi waliotoa maoni yao kuhusu hatua hiyo ya Serikali ya Kenya ambapo amesema……..

Uamuzi huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila vikwazo.

Gesi ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa kupitia bandari ya mombasa.

Uamuzi wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.

Uamuzi huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi hiyo.

Ninamsihi Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa nafuu kutoka Tanzania. Viwanda vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo cha bidhaa zilizoongezwa thamani.

Serikali ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam. Kama Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue msimamo kama huo kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye soko letu.

VIDEO: Alichozungumza JPM kwenye sherehe za muungano Dodoma, Bonyeza play hapa chini kutazama

 

You Might Also Like

Kamati ya Bunge ya Miundombinu imeridhishwa na ujenzi wa BRT

Waziri Mkuu awataka vijana na Wanawake kuchangamkia program ya IMBEJU

AudioMPYA: Joshua Ngelendo anakualika kusikiliza “Jemedari”

List ya Wasanii wakubwa watakaoimba Tamasha la Pasaka 2023

TCDC na Makakati kukuza biashara kidijitali

TAGGED: Zitto Kabwe
Edwin Kamugisha TZA April 26, 2017
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Matano ya Ray Kigosi kwa Diamond na Kanumba kudaiwa kuwa Freemason
Next Article VIDEO: Waandishi walioshambuliwa kwenye vurugu za CUF wasimulia
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Madiwani (3) Waandamanaji 87,wakamatwa nchini Afika ya kusini.
Top Stories March 20, 2023
Jela kwa mauaji,kuchomoa moyo na kuupika kulisha familia yake “Ninawaondolea mapepo” .
Top Stories March 20, 2023
Tunisia yaadhimisha Miaka 67 ya Uhuru.
Top Stories March 20, 2023
Serikali ya Taliban yapiga marufuku zao la bangi.
Top Stories March 20, 2023

You Might also Like

Top Stories

Madiwani (3) Waandamanaji 87,wakamatwa nchini Afika ya kusini.

March 20, 2023
Top Stories

Jela kwa mauaji,kuchomoa moyo na kuupika kulisha familia yake “Ninawaondolea mapepo” .

March 20, 2023
Top Stories

Tunisia yaadhimisha Miaka 67 ya Uhuru.

March 20, 2023
Top Stories

Video: Jamaa atumia dakika 8 kula Wali na nyama kilo mbili

March 19, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?