Top Stories

Ziwa Tanganyika limejaa maji, Shule, Zahanati zazingirwa na maji “hali ni mbaya watu wamehama” (+video)

on

Shule ya Msingi Mgumile iliyopo Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma/Ujiji imezingirwa na maji ya Ziwa Tanganyika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi March na kufanya Manispaa hiyo kuanza na ujenzi wa madarasa ya muda.

AyoTV na millardayo.com imezungumza na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu Mwailwa Pangani alipokuwa akikagua hatua za ujenzi na ukamilishaji wa madarasa hayo ya muda amesema maji hayo yalizingira Shule baada ya likizo iliyotangazwa nchini kutokana na Ugonjwa wa Corona hali ambayo mwanzoni walidhani maji yangepungua na kuisha miundombinu ikiwa salama.

“WAFUKUZENI KAZI HAWAFAI WANATOZA HELA KUBWA” BASHUNGWA AAGIZA KWA SIMU

Soma na hizi

Tupia Comments