Michezo

Kauli nane za kuchekesha alizowahi kuziongea Zlatan Ibrahimović zipo hapa mtu wangu..

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden ambaye anaichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimović ni moja kati ya wachezaji wenye majibu ya kushangaza wanapofanya mahojiano na vyombo vya habari, Zlatan Ibrahimović ana majibu na uamuzi wa kujiamini sana. October 3 naomba nikusogezee kauli za kuchekesha ambazo amewahi kujibu Zlatan Ibrahimović.

1- Kuna wakati aliwahi kuulizwa kuhusu aina ya uchezaji wake ya Kisweden au Yugoslavia?

download (5)

Hii ni Zlatan Style

2- Alipata nini mke wake katika siku yake ya kuzaliwa?

download (6)

Hakupata kitu kwa sababu tayari alikuwa na Zlatan

3- Alipokeaji matokeo ya timu yake ya taifa ya Sweden kutolewa katika michuano ya Euro 2012?

download (7)

Nilienda mapumziko ya msimu tu

4- Wakati alipoulizwa na ripota kuwa yeye alikuwa shoga?

download (8)

Njoo nyumbani kwangu na dada yako na mtoto wako nitakuonesha nani shoga

5- Kuna tetesi kuwa kanunua gari aina ya Porsche moja kati ya gari zenye kasi

download (11)

Sio kweli ila nimeagiza ndege ambayo itakuwa na kasi zaidi

 

 

6- Ni msichana gani ambaye anafikiria kuwa ni mrembo za duniani

download (13)

Bado sijakutana nae lakini kama ikitokea nikakutana nae nitakuwa nae katika mahusiano ya kimapenzi

7- Vipi ulipata nafasi ya kujiunga na Arsenal nini kilitokea mipango hiyo ikafa

download (14)

Arsene Wenger aliniomba kwenda kufanya majaribio na Arsenal, nilikataa kwa sababu Zlatan sio mchezaji wa majaribio.

8-  Kwa nini kuna makovu katika sura yake?

download (12)

Sifahamu unatakiwa kumuuliza mkeo kuhusiana na hilo

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments