Ni wazi sasa mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayekipiga katika klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic hana mpinzani na atakumbukwa kwa muda wote kutokana na rekodi yake aliyoiweka muda wote, tuliwahi kusikia kuwa mashabiki wa soka wa Sweden kutokana na kumpenda na kumuheshimu Zlatan Ibrahimovic mashabki wa soka Sweden wangependa kumuona sura yake ikiwa katika hela ya nchi hiyo (Krona) sema sheria hairuhusu.
Zlatan ametangazwa kwa mara nyingine tena kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Sweden na kupewa tuzo ya mchezaji bora kwa mara ya tisa mfululizo, kwa ujumla Zlatan Ibrahimovic ametwaa tuzo hiyo mara kumi na kwa mara ya kwanza alitwaa tuzo hiyo mwaka 2005 na mwaka 2007 ndio alianza kutwaa mfululizo.
Staa huyo wa PSG bado ameendelea kuwa na mwaka mzuri baada ya mwaka uliyopita kutwaa taji la Ligi Kuu Ufaransa na kutimiza jumla ya Makombe 12 ya Ligi Kuu katika maisha yake ya soka sambamba na kufunga magoli 30 katika mechi 35 alizocheza msimu uliyopita.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.