Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya April 26 2017 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari sita ‘Hot‘ kupitia TV za Tanzania.
Habari ya Clouds Tv – Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Dodoma
Rais Dkt Joh pombe Magufuli ameongoza maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma huku akionya wanaojaribu kuuchezea kwa lengo kuuvunja muungano huo uliosisiwa April 26 1964 na Marais hayati Mwl.Nyerere na Shekhe Aman Abed Karume.
Habari ya Chanel 10 – Mwanza waadhimisha Muungano kwa kufanya usafi.
Katika kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Taasisi mbali mbali za serikali na wadau wa mazingira Leo April 26 2017 wameungana kufanya usafi katika wilaya ya Nyamagana Ilemela ambapo pamoja na mambo mengine mengi serikali imeahidi kuapambana na waalifu.
Habari ya Chanel 10 – Tamko la jukwaa la wahariri Tanzania
Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) limelaani tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa waandishi wa habari lililotokea wakati wakitekeleza majukumu yao katika mkutano ulioitishwa na viongozi wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Kinondoni wiki iliyopita.
Habari ya Clouds – Gambo hataki mzaha Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake katika wilaya ya Arusha mjini na kumuagiza mkurugenzi wajiji kuepuka wakandarasi wanaopata miradi kwakudai asilimia kumi hali ambayo inasababisha miradi mingi kutekelezwa chini ya kiwango.
Habari ya Clouds Tv – Asha anayeishi na mateso ya Saratani
Mkazi wa Kinzudi wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Asha mwenye umri wa zaidi ya miaka 45 anaishi kwa mateso makali kutokana na saratani ya titi ambayo imesababisha titi lake lakushoto kukatika huku akikosa huduma ya matibabu.
Habari ya Azam Two – Wafuasi wa Guleni wasakwa Uturuki
Polisi nchini uturuki wamefanya upareshioni ya wakati mmoja nchini humo kwa kuwakamata mamia ya watu kwa tuhuma za kuwa na mawasiliano na kiongozi wa dini Guleni anayeishi Marekani na kamata kamata hiyo imekuwa sehemu ya msako wa nchi nzima kufuatia jaribio lakuiyangusha serikali ya nchi hiyo toka mwaka jana.
VIDEO: JPM akizungumza kwenye sherehe za Muungano Dodoma