Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi ‘ZNZ Heroes’ wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume wakitokea kisiwani Pemba palipokuwa panafanyika Mashindano ya kuadhimisha Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar ambapo wamepokelewa na Waziri wa Habari Vijana Sanaa Utamuduni na Michezo Zanzibar Mhe Tabia Maulid Mwita
Zanzibar Heroes wanatarajiwa kuelekea Ikulu ya Zanzibar, Mnazi Mmoja kushiriki Hafla ya chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo Januari 15. 2025