SERIKALI imeagiza kuwa zoezi la ulipaji fidia ya sh, bilioni 6.2 kati ya sh, bilioni 14.48 kwa Wananchi 595 kutoka vijiji vinne vya Engaruka Chini, Mbaash, Idonyonado na Irerendeni.
Kata ya Engaruka Wilayani Monduli kwa ajili ya kupisha Mradi wa Magadi Soda likamilike ifikapo Februari 15, 2025.
Akizungumza na Wananchi wa Eneo hilo Januari 2023 kwa niaba ya Rais Samia Hassan Suluhu wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la ulipaji fidia , Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt, Selemani Jafo alisema fedha hizo za fidia zimetolewa ikiwa ni Mkakati wa kutekeleza Miradi huo wa Kielekezo wenye manufaa makubwa katika kuendeleza sekta ya viwanda, kuongeza ajira, kukuza Pato la Taifa na uchumi kwa ujumla .
Aidha, ameliagiza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC ) kuhakikisha ulipaji huo unatetendeka kwa haki na kufuatilia malalamiko yote ya wananchi yakayojitokeza kushughulikiwa ipasavyo, kuandaliwa kwa mipango miji itakayoruhusu ujenzi wa hoteli na huduma nyingine za jamii huku akiwataka Wananchi kuchangamkia fursa zitakazojitokeza kupata ajira na na kuendeleza biashara.
Vilevile, alilisisitiza Shirika hilo kusimamia upatikanaji wa Wawekezaji wenye sifa na uwezo na si makanjanja ili Mradi huo ulete manufaa kwa Taifa na Wananchi kwa kurahisisha upatikanaji wa malighafi hiyo nchini na kuokoa fedha nyingi za kigeni zilizokuwa zinatumika kuagiza malighafi hiyo nje ya nchi.
Aidha amewasisitiza Wananchi kupuuza Taarifa potofu ambazo zimekuwa zikienezwa na watu ambao hawaitakii mema nchi yetu kwa kuwa NDC ambao ndio watekelezaji wa mradi huu wamekabidhiwa Cheti cha Ithibati za mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kinachothibitisha kuwa uchimbaji wa magadi soda katika Eneo la Engaruka hauna athari zozote za kimazingira kwa ndege ain flamingo ambao hawapo eneo hilo.
Dkt Jafo pia amebainisha kuwa Serikali imeweka mpango wa kukahakisha eneo la Engaruka barabara zake zinapitika pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa umeme mkubwa KV 33 kwa ajili ya kuendesha viwanda sanjari na upatikanaji wa huduma za kijamii katika sekta za elimu, afya na maji safi na salama.
Aidha, Viongozi mbalimbali walioshiriki Hafla hiyo wamesema kuwa Mradi hiyo uliosubiriwa kwa miak takribani 20 utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo katika eneo hilo la Engaruka, Arusha na Taifa kwa ujumla.
Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geofrey Pinda amesisitiza kuwa Wizara yake itashirikiana na Wananchi wa Wilaya za Longido na Monduli kuweka mipaka na kuwa na mipango bora ya matumizi ya Ardhi katika vijiji vya Engaruka ili kuepuka migogoro kwa kushirikiana na kamati za vijiji.
“Wananchi wasigombanishwe na migogoro ya mipaka kati ya Wilaya za Longido na Monduli wekeni mipaka ili maendeleo yapatikane na wizara hii itatoa ushirikiano saa zote na RC Makonda pale unapoona panakero tuwasiliane ili kutatua migogoro ili wananchi waishi kwa amani ”
Vilevile, amewaelekeza Maafisa Ardhi katika Wilaya ya Monduli na Longido kushiriki kikamilifu katika zoezi la kurejesha mawe ya mpaka ya wilaya hizo mbili yaliyong’olewa na kupoteza utambuzi wa mpaka huo.