Msanii wa Afropop na Bongo Flava kutoka Tanzania Zuchu ndiye balozi mpya kwa mwezi wa Mei, wa program ya muziki iitwayo “EQUAL Africa” kinacho endeshwa na Spotify. Lengo la programu ya “EQUAL” ni kuimarisha usawa wa kijinsia katika muziki kwa kuwaonyesha wanawake wa Ki-Afrika wenye vipaji wanaotikisa mawimbi katika tasnia hiyo na kutoa jukwaa la kuwaenzi.
Tangu kuzinduliwa kwake katika siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani mwaka 2020, Spotify imekua ikiendesha programu ya EQUAL kila mwezi ambapo wasanii wa kike mbalimbali huangaziwa kutokana na vipaji na umahiri wao katika tasnia ya muziki. Kila mwezi, msanii wa kike huchaguliwa kuwa Msanii wa EQUAL na mojawapo ya nyimbo zake kutumika kama kichwa cha nyimbo za EQUAL Africa.
Baadhi ya wasanii ambao wameangaziwa hadi sasa ni pamoja na Tiwa Savage wa Nigeria, Fave, Ayra Starr na Asa; DBN Gogo wa Afrika Kusini na Nomfundo Moh; na Gyakie na Amaarae wa Ghana. Vilevile, Zuchu anaungana na nyota wa Afrika Mashariki Muthoni Drummer Queen, Malkia wa Kenya na Silvia Sssaru katika kukuza sauti za wanawake wa Kiafrika wenye vipaji kupitia EQUAL.
Akiwa mzaliwa wa familia ya kimuziki na kwa sasa akiwa amesajiliwa na rekodi ya Diamond Platnumz ya WCB, Zuhura Othman Soud (almaarufu kama Zuchu) ni mtoto wa mwanamuziki nguli wa Taarab, Khadija Kopa, ambaye aliimba naye wimbo wa “Mauzauza.”
Zuchu aliingia kwenye ulingo wa muziki kwa mara ya kwanza mwaka 2015 kupitia shindano la kutafuta vipaji lenye mada ya karaoke mjini Lagos, Nigeria. Kisha mwimbo wake maarufu wa “Cheche” aliomshirikisha Diamond Platnumz ukamzulia umaarufu mnamo 2020. Mwaka uliofuata, alitoa wimbo uliovunja rekodi, “Sukari,” ambao umepata wasikilizaji zaidi ya milioni 2 wa Spotify.
“Mbali na kunionyesha uwezo wa kimuziki unaoweza kutoka kwa uzoefu wa wanawake katika muziki, program hii pia imenisaidia kutambua kwamba tunaweza kushinda vikwazo ambavyo ni sehemu ya kufanya kazi katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume wa Afrobeats, ” asema Zuchu akiwakumbuka wanamuziki wote wa kike ambao wamemtia moyo katika safari yake.
“Kuwa sehemu ya programu ya “EQUAL”, ni jambo kubwa kwangu na inasaidia kuhimiza wanamuziki wengine wa kike kuvumilia na kuvunja vizuizi vya jinsia katika nyanja ya muziki,” anaongeza.
Wimbo mmoja wa Zuchu “Mwambieni“, uliotolewa mapema mwaka huu, umeangaziwa kwenye orodha za kucheza za EQUAL Africa na EQUAL Global kwenye Spotify.
“Tunafuraha kubwa kwa Zuchu kajiunga na program ya EQUAL. Ni dhahiri kuwa ni mmoja wa wasanii wenye vipaji vingi kutoka Tanzania, na hii ni sifa anayostahili,” anasema Phiona Okumu, mkuu wa muziki wa Spotify Kusini mwa Jangwa la Sahara akiongeza kuwa Spotify imejitolea kuwaangazia wasanii wa kike barani Afrika kwa matumaini kwamba mpango huu utawahamasisha wasanii wengine wachanga na wajao katika tasnia ya muziki kudumu kwenye njia sahihi na kuendelea kufanya kile wanachofanya.