Top Stories

Zuma aruhusiwa kumzika mdogo wake

on

Rais wa zamani wa Afrika kusini Jacob Zuma amepewa ruhusa ya kushirikia maziko ya mdogo wake Michael anayetarajiwa kuzikwa leo mchana.

“Kwakuwa ni mfungwa wa kifungo cha muda mfupi, mwenye hatari ndogo ya kutoroka, ombi la Zuma la kuomba ruhusa ya msiba limekubaliwa” amesema Msemaji wa idara ya kurekebisha tabia Singabakho Nxumalo mapema hii leo.

Kwa mujibu wa Nxumalo,  Zuma hatolazimika kuvaa sare za wafungwa atakapokuwa msibani.

Jacob Zuma anatumikia kifungo cha miezi 15 gerezani baada ya kukaidi amri ya kuhudhuria mahakamani kwenye kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na rushwa inayomkabili.

Wafuasi wa Zuma walifanya maandamano na vurugu ikiwemo uporaji na uchomaji moto mali mbalimbali kwa wiki mbili kupinga hukumu ya kifungo cha miezi 15 alichohukumiwa Zuma.

MTOTO MDOGO WA GIFT ALIYEUAWA ASIMULIA ALICHOAMBIWA NA BABA YAKE KABLA HAJAFA, MAMA ATOA YA MOYONI

Soma na hizi

Tupia Comments