Timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Karume Boys April 16 2018 imechukua headlines baada ya chama cha soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA kutangaza kuifungia Zanzibar kwa kipindi cha mwaka mmoja kushiriki michuano ya CECAFA.
Zanzibar imetangazwa kufungiwa baada ya kubainika kikosi chao kuwa na wachezaji 12 waliyovuka umri wa kushiriki mashindano hayo kitu ambacho ni kinyume na taratibu za mashindano hayo yanayowataka washiriki vijana pekee wenye umri wa chini ya miaka 17.
Hata hivyo Zanzibar imeondolewa katika michuano hiyo na kupigwa faini ya dola 15000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 30 kama fidia ya gharama ya timu hiyo iliyotumia ilipokuwa Burundi, Ethiopia nao wamepigwa faini ya dola 5000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 10 kwa kukutwa na wachezaji watatu waliyozidi umri.
ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1
https://youtu.be/-X6tg5a15HI