Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

VIDEO: Kauli ya Mwisho ya Kocha wa Taifa Stars “Nimewaandaa kisaikolojia”

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo mazoezi yake ya mwisho jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Harambee Stars wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika (CHAN 2020) zitakazofanyika nchini Cameroon, baada ya  mazoezi hayo AyoTV ilifanikiwa kuinasa kauli ya mwisho ya kaimu kocha mkuu Etienne Ndairagije kabla ya kucheza game hiyo.

“Kama tulivyosema mazoezi yamekuwa ya mwisho ya kuangalia hali ya afya ya wachezaji, kuwaona wako vizuri na tulichukua nafasi hii ya kuangalia uwanja na kuongea hasa kwa sababu hii ni mechi ambayao inahitaji kujiandaa kisaikolojia kwa sababu tunatumia nguvu nyingi, tunaimani kuwa maandalizi yameenda vizuri na kila kitu kimekuwa sawa”>>>Ettiene

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa marudiano na Harambee Stars Jumapili ya August 4 2019, hiyo ni baada ya mchezo wao wa kwanza kumalizika kwa sare 0-0, Taifa Stars ili isonge mbele itahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kufungana magoli.

VIDEO: Erasto Nyoni kagusia kikao chao cha Manahodha (Bocco, Kaseja na Yeye) leo

Soma na hizi

Tupia Comments