Michezo

Neymar akiri akicheza na Hazard wataleta shida

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea club ya PSG ya Ufaransa Neymar, ameonesha nia yake ya kutaka siku moja kucheza katika timu moja na staa wa Chelsea Eden Hazard, staa huyo wa Brazil anaamini akicheza na Hazard watasumbua sana.

Neymar aeleza kuwa anavutiwa sana na uchezaji wa Eden Hazard na kusema uchezaji wao kama unataka kufanana kidogo, hivyo wakicheza timu moja basi watasumbua sana timu pinzani, pamoja na hayo Neymar amewahi kuhusishwa kuhitajika na Real Madrid kama ilivyo kwa Hazard na ikitokea mastaa hao wakajiunga na Real Madrid itakuwa fursa kwao kucheza pamoja.

“Ningependa kucheza na Hazard ni mchezaji wa kipekee anacheza kidogo kama mimi ninavyocheza, ningependa kucheza nae timu mmoja, nafikiri tungesumbua sana timu pinzani kama tungekuwa tunacheza timu moja”>>>>Neymar

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments