AyoTV

VIDEO: Wanayoyataka ACT-Wazalendo baada ya Serikali kuwarudisha wanafunzi wa UDOM

on

August 3 2016 Umoja wa vijana chama cha ACT-Wazalendo umekutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kuzungumzia changamoto zilizopo katika sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja kitendo kilichofanywa na serikali kwa kuwasimamisha masomo wanafunzi wa Chuo kikuu Dodoma (UDOM) wasiokuwa na sifa na baadae kuwarudisha baadhi yao.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao Kitentya Luth ambaye ni mratibu wa vijana ACT-Wazalendo amesema wanataka ufafanuzi wa Serikali kuhusu ukweli kwamba ilifanya hivyo kwa mashinikizo matatu ikiwa ni pamoja na kukosa fedha za wafadhili.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao Kitentya Luth ambaye ni mratibu wa vijana ACT-Wazalendo amesema…>>>‘Katika uamuzi huo wa kuwafukuza watoto wa kimaskini kutoka UDOM kukaibuliwa lugha za udhalilishaji kwa kuwaita Vilaza bila kuangalia athari za kisaikolojia

Sisi kwa nafasi yetu kama vijana tunalaani vikali udhalilishaji huo mbali ya kulaani tunaitaka Serikali ituambie na kutujibu masuala matatu yakiwemo‘ –Kitentya Luth

  1. Je, ni kweli tatizo lilikuwa Udahili ambao haukukidhi vigezo au ni ukosefu wa fedha baada ya wafadhili kujitoa kama tunavyosikia?
  2. Mliwezaje kuwapata wanafunzi zaidi ya 300 mkidai wamekidhi  vigezo vya kurudi chuo na tunafahamu 7000 walikosa sifa kwa matokeo yao kuwekwa hadharani?
  3. Serikali imewapeleka wanafunzi katika vyuo vingine, je, waliopelekwa walienda kuendelea na elimu waliyoanza awali au walikuwa na mwanzo mwingine

ULIIKOSA HII SABABU ZA MREMA KUAMUA KWENDA KUMUONA RAIS MAGUFULI

Soma na hizi

Tupia Comments