Habari za Mastaa

Hatimae Ben Pol akutana na Ebitoke, ‘Wengi wameoa, kuolewa na wasiowapenda’

on

Moja ya story kubwa ambayo ilimake headlines siku kadhaa zilizopita ni kuhusu Mchekeshaji Ebitoke kuweka wazi hisia zake kuwa anampenda staa wa RnB Tanzania Ben Pol akimuomba waonane na ikiwezekana wafunge ndoa akisema anajitunza kwa ajili yake.

Sasa leo June 23, 2017 kupitia Instagram yake Ben Pol ameweka picha akiwa na Ebitoke na kuweka maneno ambayo yanaelezea hisia zake pia kwa kilichofanywa na mchekeshaji huyo kwa kuheshimu hisia zake.

“Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika?

“Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, labda huyo Mtu kesho hatokuwepo.

“Ebitoke umenifundisha jambo KUBWA SANA maishani, najua wengi walikubeza sana , wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na Mimi.. lakini huwezi amini Mimi nimefurahi mno!! kukutana na wewe na kuongea, na nimepata jambo kubwa sana. Na Nitayaishi Maneno yako ???. Nakushukuru sana, Mwenyezi Mungu akuzidishie. You are THE BEST ??!!@ebitoke #blessed??” – Ben Pol.

VIDEO: Mchekeshaji Ebitoke aahidi kujitunza kwa ajili ya Ben Pol 

ULIPITWA: Ben Pol afunguka kuhusu picha zake za bila nguo 

Soma na hizi

Tupia Comments