Michezo

Jose Mourinho kamvulia kofia Cristiano Ronaldo

on

Kocha wa zamani wa club za Man United, Chelsea pamoja na Real Madrid Jose Mourinho ameeleza mtazamo wake kuhusiana na uwezo wa staa wa Juventus ambaye pia ni raia mwenzake wa Ureno Cristiano Ronaldo kuwa ana uwezo wa viwango vya juu katika soka kutokana na umahiri wake wa kufunga.

Mourinho ameeleza hayo  huku akisifia kuwa Ronaldo ana uwezo wa hali ya juu na kiwango cha kipekee, hata wakati atakapostaafu soka na kufikisha umri wa miaka 50 bado akiwa kaalikwa katika mechi za legends anaweza kuwa anafunga tu, hiyo ni baada ya Ronaldo kufunga magoli 4 katika mchezo wa kuwania kufuzu Euro 2020 dhidi ya Luthania.

“Ameweka alama ni mtu fulani anayefikiria kuhusu kushinda na kufanya zaidi kwa ubora, ndio maana huwa sishangazwi kwa anachokifanya kila siku, wakati atakapokuwa na umri wa miaka 50 atakuwa nyumbani na FIFA watakuwa wanamualika katika mechi za ma-legends, atacheza na kufunga magoli, nina uhakika itakuwa kama hivyo”>>> Jose Mourinho

Weekend iliyomalizika ya game za kalenda ya FIFA Cristiano Ronaldo kaingia kwenye headlines baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ulaya kufunga magoli 90 katika michezo ya kimataifa akifuatiwa na Ferenc Puskas mwenye magoli 84 akiwa amestaafu soka toka 1962.

EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE

Soma na hizi

Tupia Comments