Michezo

Iran imewaondoa timu ya taifa wachezaji wenye tattoo

on

Habari kubwa katika soka leo wakati huu wa mapumziko wa Ligi mbalimbali duniani kwa sababu ya kupisha mechi zilizopo katika kalenda ya FIFA, Tehran Times wameripoti kuwa imetolewa taarifa rasmi nchini Iran kuwa wachezaji wa taifa hilo ambao wamechora tattoo katika miiwili yao hawana nafasi.

Inaelezwa kuwa shirikisho la soka Iran limepewa agizo kuwa la kutowaita kikosini wachezaji waliochora tattoo katika miili yao, siku kadhaa zilizopita shirikisho la soka la Iran lilikuwa limeagiza wachezaji wenye tattoo wavae jezi za mikono mirefu katika michezo yao ya club.

Uamuzi huo umekuja kutokana na Iran uchoraji wa michoro kwa watu mwilini maarufu kama tattoo ni kinyume cha maadili yao, hivyo kwa sasa hawatokuwa na nafasi tena wachezaji wa Iran waliyokuwa wamechora tattoo, kwa upande wa Ulaya wachezaji kama Lionel Messi, Sergio Aguero na Zlatan Ibrahimovic ni miongoni mwa wachezaji wenye tattoo.

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments