Habari za Mastaa

EXCLUSIVE: Mubenga kafunguka ishu ya Ommy Dimpoz kumpost mama Diamond

on

Inayotajwa kuwa ne beef kati ya mastaa wa Bongofleva Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz imezidi kuchukua sura mpya hasa baada ya Ommy Dimpoz kumpost mama Diamond kwenye Instagram jambo lililowashtua wengi.

Meneja wa zamani wa Ommy Dimpoz, Mubenga ni mmoja walioonesha kuumizwa na kitendo hicho ambapo Ayo TV na millardayo.com zimefanikiwa kukaa naye kwenye EXCLUSIVE na kufunga zaidi namna alivyojisikia baada ya Ommy Dimpost kumpost mama Diamond.

>>>“Kweli nikiwa kama Mtanzani sikupenda kile ambacho kimetokea. Kwa sababu ukizingatia mama ni Mungu wa pili duniani, so sikuona haja ya Omary kufanya kile alichokifanya. Kama aliona Mondi amemkosea basi ni bora na yeye angerudi kumzungumzia Mondi mwenyewe na siyo mama yake.”Mubenga.

Soma na hizi

Tupia Comments