Leo April 26, 2018 watu wa Uganda watakuwa na mkesha wa kuomboleza kifo cha Sokwe mkubwa zaidi nchini humo ambaye amekufa akiwa na miaka 54 na kituo cha elimu ya hifadhi ya wanyamapori kimesema kuwa alitunzwa na wataalam na baadae alifikishwa kwenye hifadhi ya taifa akiwa na miaka 13.
Sokwe huyo mwenye jina la Zakayo ambaye alizaliwa mwaka 1963 alichukuliwa na Kituo Cha Elimu ya hifadhi Wanyamapori nchini humo na aliishi sana katika hifadhi ya Entebbe na hapo awali kwa mujibu wa mamlaka nchini humo, alikuwa hatarini kwani watalii walikuwa wakimpa sigara na pombe ili awafurahishe.
Pamoja na hilo imeelezwa kuwa mabaki ya Sokwe huyo yatatunzwa kwa ajili ya utafiti na elimu.
Ilivyokuwa Uzinduzi wa Movie ya Avenger Infinity War Mliman City DSM
Dodoma imekuwa JIJI Ben Pol kazungumza haya
MC Pilipili baada ya Dodoma kuwa Jiji “Tulikuwa tunaogopa kusema unatoka Dodoma”