Utafiti uliyofanywa hivi karibuni kutoka majiji kadhaa makubwa duniani umeonyesha kwamba kumekuwa na unyanyasaji wa kutisha wa Wanawake katika vyombo vya usafiri.
Utafiti huo uliofanywa na mfuko wa Thomson Reuters Foundation umeonyesha Wanawake sita kati ya kumi katika majiji makubwa huko Latin America wameripotiwa kunyanyaswa wakati wakiwa ndani ya vyombo vya usafiri wa abiria ambapo Bogota, Colombia imetajwa kuwa hatari zaidi ikifuatiwa na jiji la Mexico na Lima Peru.
Nchi ya Japan imeingia katika orodha ya moja ya majiji hatari kwa Wanawake wanaotumia vyombo vya usafiri wa abiria duniani ambapo utafiti huo uliofanywa katika majiji 15 makubwa duniani, jumla ya Wanawake 6,500 walihojiwa na majibu yaliyopatikana ni kama yanavyoonekana kwenye orodha hii;-
1. Bogota, Colombia
2. Jiji la Mexico, Mexico
3. Lima, Peru
4. New Delhi, India
5. Jarkata, Indonesia
6. Buenos Aires, Argentina
7. Kuala Lumpur, Malaysia
8. Bangkok,Thailand
9. Moscow, Russia
10. Manila, Philippines
11. Paris, Ufaransa
12. Seoul, Korea Kusini
13. London, Uingereza
14. Beijing, China
15. Tokyo, Japan