Kuna ripoti mpya ya shirika la Amnesty International imetoka ambapo nchi za Iran na Iraq zimeongoza katika kutekeleza adhabu za kifo duniani ambapo mwaka jana peke yake asilimia 66 ya walionyongwa ilikua kwenye hizi nchi.
Japo kuwa nchi chache sana zinatumia adhabu ya kifo duniani ukilinganisha na miaka 20 iliyopita, kuua wahalifu Iraq na Iran kumesaidia kuongezeka kwa asilimia 15 za adhabu za mauaji duniani.
Kuna watu 778 ambao wameuliwa kutokana na adhabu ya kifo duniani kwa mwaka 2013 pekee ambapo kwenye hiyo idadi, 538 ni ya Iran na Iraq pekee ambapo rekodi ya dunia nzima kwa mwaka 2012 ilikua 682 huku shirika hili likisisitiza kwamba mauaji ya uhalifu waliyoona katika nchi kama Iraq na Iran yalikuwa ni ya aibu.
Kwa nchi kama China ambayo imewahukumu kunyongwa Watanzania 15 kati ya 177 waliofungwa gerezani sasa hivi, wanaaminika kutoa adhabu ya kifo kwa maelfu ya watu kwa mwaka ikiwa ni zaidi ya hesabu ya dunia nzima lakini hakuna takwimu halisi juu ya hilo kwa sababu mamlaka yao Beijing inasema takwimu hizo ni siri ya taifa.
Kwa Iran, orodha iliyotoka 2013 ni ya watu 369 ikiwa imeongezeka watu 55 kutoka 2012 ambapo hata hivyo inaaminika mamia ya watu wengine wamepewa adhabu hiyo kisiri.
Iraq wametoa adhabu kwa watu mpaka 169 ongezeko ya nusu na robo kutoka mwaka 2012, Saudi Arabia imetoa adhabu hiyo kwa watu 79 na Marekani ni watu 39 tu.
Kwa upande wa Africa, Benin, Ghana na Sierra Leone wamechukua hatua za kuanza kusitisha adhabu hii, Somalia imezidisha adhabu hii ambapo wameuwa watu 34 mwaka 2013 kutokana na adhabu ya kifo, na 6 tu mwaka 2012.
Na kwa Marekani bado inaendelea kutumia adhabu hizo ambapo wengi walioadhibiwa wanatoka jimbo la Texas.
Korea Kaskazini pia haina orodha kamili lakini inasemekana imekua ikitoa adhabu ya kifo kwa watu wenye makosa ya dawa za kulevya, uasherati, kufuru na uenezaji wa picha za ngono na pia wamekua wakiua watu kwa makosa ya kuangalia video zisizoruhsiwa (banned videos) zinazotoka nchi jirani ya Korea Kusini.
Ripoti hii inasema zaidi ya watu 23,000 walikuwa katika orodha ya kuuwawa kwa adhabu ya kifo mwaka 2013 na watu 2,000 walikuwa wameshapewa hukumu ya kifo katika nchi 57 mwaka 2013.
Orodha ya nchi kumi kwenye hii adhabu ya kifo ndio hii hapa chini