Wataalamu wa mambo wanasema kwa jinsi mji wa Kigali unavyojengwa majengo ya kisasa wakati huu, miaka 10 baadae sifa itaongezeka maradufu kwenye list ya miji ya Afrika inayotolewa sana mifano ya kuigwa Afrika.
Pamoja na hayo, ni mji ambao ni msafi sana kimazingira, kuna usalama wa hali ya juu na ndio maana sio kitu kigeni kukutana na askari kwenye kila kona lakini pia vilevile sheria zinatekelezwa sana ambapo rushwa haina nafasi kabisa.
Usalama wa kutembea usiku pia ni mkubwa sana, niliwahi kuingia night club na kutoka saa tisa na nusu na barabarani kukawa kuna askari wa kutosha kila kona, nilipouliza kwanini kuna watu bado wanatembea kwa mguu pembeni mwa barabara ndio nikapewa stori mwanzo mwisho jinsi ulivyo mkali.
Kingine nilichojifunza ni kwamba sheria ni kali hata kwa watu wa bodaboda, yeyote anaweza kujuta sana pale atakapokamatwa hajavaa helment.
Kuna chochote ungependa kuchangia kwa maoni baada ya kuona hizi picha? niandikie kwenye comments hapa chini mtu wangu…
Kila kinachonifikia ni halali yako kikufikie na wewe mtu wangu, karibu ujiunge na mimi kwa kubonyeza hapa >> Twitter Instagram facebook