Nafahamu kuwa nina watu wangu wa nguvu wanaopenda michezo mbalimbali hasa kandanda ndiyo maana DStv wamenifikishia good news ambayo napenda pia nawe ikufikie.
Naambiwa Watanzania wameendelea kuhakikishiwa wataendelea kufuatilia mashindano makubwa Duniani baada ya DStv kupitia SuperSport kuingia makubaliano ya kurusha mashindano makubwa ya kimataifa, ikiwemo mashindano ya Ulaya maarufu UEFA Euro mwaka 2020 katika makubaliano ambayo yatawahakikishia watazamaji wa DStv kushuhudia michuano yote mikubwa ya soka kila msimu hadi 2022.
Mbali na kuzishuhudia fainali za UEFA Euro, pia Watanzania watakuwa na nafasi ya kushuhudia hatua za awali yaani kufuzu UEFA Euro 2020 na kufuzu Kombe la Dunia 2022 itakayopigwa Qatar huku yakiwepo pia mengi ya kufurahia kwa watazamaji wa DStv kwa kuwa SuperSport wataendelea pia kuonesha msimu mpya wa Ligi ya UEFA.
Wagombea 57 wamejitokeza kuwania uongozi TFF!!!