Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali ameitaka Serikali ikiwemo Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika wa matukio ya kiuhalifu ambayo Serikali imekuwa ikiyakalia kimywa na kusababisha kuchafuliwa.
“Kuna mambo yanafanyika nchini kwetu mimi natafsiri kama ni fedheha kwa jeshi la Polisi, Kuna bwana mmoja alimtishia Nape bastola alafu Waziri akasema huyu mtu atafutwe na tutamshugulikia lakini hadi leo kimya. Yule mtu anaonekana mtaani, hata juzi amefanya kazi mbele ya kamera, inamaana Polisi hawaoni kama haya mambo yanawachafua? ” – Peter Lijualikali
Ni kweli Mbunge Mlinga alimchoma sindano mwanafunzi? Itazame hii video