Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (CC) ya CHADEMA Edward Lowassa leo June 29, 2017 aliripoti kwa mara ya pili katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuitikia wito wa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambaye hata hivyo aliruhusiwa kuondoka kwa madai ushahidi haujakamilika.
Baada ya kutoka Makao Makuu ya Polisi Lowassa alikutana na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mikocheni, DSM na kuzungumzia juu ya issue hiyo akisema:>>>”Demokrasi ikishaanza ni gurudumu, kuizuia ni vigumu. Unaweza ukapunguza speed ya gurudumu la demokrasi lakini huwezi kuiondoa…demokrasi imeshaanza, inaendelea, ni vigumu kuizuia.
“Pili, ningetumia nafasi hii kuwaomba Wanachama wa Chama chetu na Wananchi na wanaotutakiwa mema wasiwe na mashaka kila kitu kiko chini ya utaratibu mzuri. Tuko sawasawa, tuko sahihi na tumetekeleza kama alivyosema Mwenyekiti sera ya Chama chetu. Wasiogope, wawe na amani, watulie.
“Jambo la msingi pale ni kuachiliwa Masheikh wa UAMSHO. Hatusemi hawana makosa lakini wamekaa pale miaka minne au mitatu. Nadhani ni wakati mzuri watu wale kuondolewa jela. Tulisema kwenye Ilani yetu kwamba watu hawa ni vizuri wakaondolewa gerezani, wamekaa vya kutosha.” – Lowassa
Tamko la CHADEMA mbele ya waandishi DSM!!!