Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM mkoani Dodoma Mariam Ditopile alikuwa mgeni rasmi katika kikao cha baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)kata ya Chan’gombe mkoani humo ambapo katika hotuba yake alionesha kutofurahishwa na baadhi ya viongozi wanaoshindwa kutatua kero za wananchi.
“Wenyeviti wa mitaa nyinyi ndio jeshi letu hakikisheni uchaguzi wa 2019 wa serikali za mitaa hatupotezi mtaa hata mmoja,kwenye makosa tujirekebishe ,diwani hakikisha hatupotezi mtaa wowote hapa,na katika uchaguzi mkuu tunataka kura ziongezeke kutoka zile zilizopatikana kwenye uchaguzi uliopita” –Mariam Ditopile
“Ni aibu kwa kiongozi wa CCM kukosa ajenda ya kuzungumza mbele ya wananchi wakati serikali inafanya mambo mengi ya kimaendeleo,huko ni kutoitendea haki CCM,elezeni miradi inayotekelezwa,simamieni upatikanaji wa asilimia 5 hiyo ndio kazi yenu”-Mariam Ditopile
Tanzania yatangaza ujenzi wa Reli kutoka TZ mpaka Rwanda