Tayari nimekukusanyia uchambuzi wa stori zote kubwa za magazeti ya Tanzania leo July 12, 2017 ambapo kila siku huwa nazipandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo na sasa zipitie hapa millardayo.com.
Viongozi wa dini wametakiwa kuwakemea viongozi wa Serikali wanaojihusisha na ufisadi na rushwa badala ya kukimbilia sadaka zao. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Katibu wa H'shauri Kuu ya CCM (CC), Uchumi na Fedha, Dk. Hawassi amesema mikataba mibovu ni moja ya sababu ya chama kupoteza mapato #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Serikali imetoa onyo kwa viongozi wa vikundi vya ujasiriamali kuepuka vitendo vya ubadhirifu wa fedha na mali kwenye vikundi vyao. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imefanikiwa kuwanasa wadaiwa sugu 45,590 kati ya wanufaika 238,519 ktk kipindi cha mwaka 2015/17. #Nipahse.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Wakala wa Msajili, Ufilisi na Udhamini imezitaka Mahakama kupeleka nakala za hukumu za talaka kupunguza migogoro ya ndoa, mirathi #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
"Tumedhamiria kuhakikisha kila aliyekopa kama hajafariki dunia lazima arejeshe fedha anazodaiwa." – Abdul-Razaq Badru. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Mamlaka ya Mapato Tanzania imeweka wazi makusanyo yake ya fedha kwa kipindi cha mwaka 2016/17 ikikusanya Tsh. trilioni 14.4. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi imesema kuna ubadhirifu katika umiliki wa ardhi na ushiriki mdogo wa wanawake. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Baraza la Wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya limelaani kukamatwa na unyanyasaji unaofanywa kwa Wabunge wa Upinzani. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
BAKWATA imewataka Waislamu nchini kuwa watulivu wakati likitarajia kumhoji Ustaadhi Hamza Issa aliyejitangaza kuwa Mtume. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Chama cha @ccm_tanzania Mkoa wa Singida kimesema hakuna mgombea atakayepitishwa kwa rushwa kugombea nafasi yoyote. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania imekataza kurusha angani vifaa vya kielektroniki visivyo na rubani (drones) bila kibali. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesema wadaiwa sugu ambao majina yao yamejitokeza kwenye vyeti feki lazima warejeshe mikopo. #TanzaniDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Mamlaka ya Bandari Tanzania imeagizwa kuzuia mianya ya ukwepaji kodi na tozo za bandari kuhakikisha inakusanya Tsh 1b kwa mwezi. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Walimu wa Shule ya St Anne Maria DSM wamefikishwa Mahakamani wakidaiwa kujipatia vitabu vya thamani ya Tsh. 2.1m kwa udanganyifu. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Rais Mgufuli amemteua Prof. Florens Luoga kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Jamii imehimizwa kuzingatia uzazi wa mpango ili kupata familia bora ambazo watamudu kuzihudumia katika mahitaji muhimu. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Jeshi la Polisi Mwanza linamshikilia mwanamke mmoja anayedaiwa kumuua mumewe kwa kitu chenye ncha kali kwa lengo la kurithi mali. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Dereva wa basi la abiria la AM Coach amefikishwa ktk Mahakama ya Wilaya ya Mlele, Katavi kwa kumuua Twiga wa thamani ya Tsh 33m. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
Imeelezwa mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa mradi wa mabasi yaendayo kasi (UDART), umeanza kuingia dosari kwa wabia wa uendeshaji. #RaiaMWEMA
— millardayo (@millardayo) July 12, 2017
EXCLUSIVE: Majibu ya Tundu Lissu kuhusu kumfuta uanachana Waziri Mwakyembe!!!