Mbunge wa viti maalum CCM Mariam Ditopile ameilalamikia Serikali kwa kushindwa kusimamia vyema sekta ya kilimo na kuwaacha wakulima wake wakiumia kutokana na sheria mbovu zilizowekwa na Serikali ambazo zinawaumiza wananchi ikiwemo zuio la kuuza mazao nje ya nchi na kuwasababishia hasara kubwa.
“Waziri wa kilimo naomba nikuambie wewe ni swahiba wangu lakini uswahiba huu hauuzidi ule nilionao na Watanzania, naomba niongee machungu yanayowapata na naomba niongee kwa facts. Tanzania tumevuka kwenye kilimo cha mahindi kwa ajili ya chakula pekee bali tunalima kwa ajili ya biashara” -Mariam Ditopile
“Hivi Waziri Tizeba unaenda kuwalisha matango pori viongozi wetu wakuu kwanini? Unaweka zuio la kuuza mazao nje ya nchi lakini unaruhusu mahindi ya nje yaingine hii ni kutuumiza wakulima na unataka tukauze wapi wakati hatupati lolote kutoka Serikalini. Mkulima anavuna mahindi aweze kuuza mnazuia, mahindi yanaharibikia ndani”–Mariam Ditopile
Mastaa wazungumzia Clip ya Polisi ya kukamata wanaojikoholesha (Shambulio la Aibu)