Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimekuwekea hapa kubwa za leo kutoka kwenye magazeti ya Tanzania, waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
#NIPASHE Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva na makamishina wengine watatu wanamaliza muda wao mwisho wa mwezi huu pic.twitter.com/limM5xkyWr
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#NIPASHE TANESCO yatimiza agizo la JPM la kupeleka umeme ktk kiwanda cha kutengeneza juisi na vinywaji baridi cha Bakhresa Vikindu Pwani pic.twitter.com/IsH8f3FJmT
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#NIPASHE Kingunge ameibuka na kusema kwa sasa ni vigumu kupata viongozi wa aina ya Mwl Nyerere, ambao hawatumii uongozi kwa maslahi binafsi pic.twitter.com/vmp7Vqtgnz
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#NIPASHE Zaidi ya mil 30 zadaiwa kupotea kipindi cha mwaka mmoja baada ya kubainika wanafunzi hewa 89 shule sekondari Kilangalanga Pwani pic.twitter.com/ERLwPoCi8D
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#NIPASHE Matumizi ya vifaa vya kuwalishia watoto wadogo kwa kutumia chupa za plastiki kunawaweka watoto kwenye hatari ya kupata saratani pic.twitter.com/6XAOqMbPil
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#NIPASHE Ziwa Nyasa lina aina ya samaki zaidi ya 1500, ni chache zinavuliwa kwa chakula wengi wanakamatwa na kuuzwa nje kwa ajili ya mapambo pic.twitter.com/KpYiqr0zuB
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#NIPASHE Waziri Lukuvi ameiagiza Serikali ya mkoa wa Shinyanga kupiga mnada nyumba zote zisizo na hati kuanzia mwakani pic.twitter.com/LL4k9plRKu
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#NIPASHE Watu 845 wagundulika na maambukizi mapya ya VVU Songea, imeelezwa waliambukizwa ktk kipindi cha kuanzia April hadi June mwaka huu pic.twitter.com/iPjEjHdL1P
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#NIPASHE Kipa mpya wa Kagera Sugar, Juma Kaseja amesema bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka na atahakikisha uzoefu wake unaisaidia timu pic.twitter.com/Pv4ToWXM2T
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MTANZANIA Kufungwa kiwanda cha Dangote Mtwara Forbes wataja sababu ni Kuongezeka gharama za uzalishaji na Kutozingatiwa kwa makubaliano pic.twitter.com/zx18F95aSa
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MTANZANIA TPA imesema kuwa kumekuwa na ongezeko la mizigo inayosafirishwa kwenda Rwanda ikitokea bandari ya DSM pic.twitter.com/cCA9pie6D5
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MTANZANIA Rais Magufuli ameteua mabalozi 21, kati yao wapya 15, wakiwemo wanasiasa wenye majina makubwa pic.twitter.com/po845gIC7D
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MWANANCHI Imeelezwa kuwa mwezi December kuwa na mauaji, ajali nyingi, chanzo ni pilikapilika za sikukuu na harakati za kujiongezea kipato pic.twitter.com/fWJasyURmp
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MWANANCHI Mke wa mbunge Lema asema yeye na watoto hawajutii kutokuwa na Lema ambaye yuko mahabusu kwa kuwa anapigania haki ya kidemokrasia pic.twitter.com/We5OLb58d0
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MWANANCHI TPA yasisitiza kuendelea na mpango wa kujenga bandari Mtwara iliyolenga kutumiwa na kiwanda cha Saruji cha Dangote na vingine pic.twitter.com/bhDtOltEol
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MWANANCHI Baadhi ya wakazi wa Kibaigwa Dodoma wanaougua kipindupindu wakwepa hospitali kutokana na imani potofu kuwa wakilazwa watarogwa pic.twitter.com/HQzyE6L8LA
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MWANANCHI Vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukizwa vinaongezeka kutokana na uvutaji wa sigara, unywaji pombe na vyakula vyenye mafuta pic.twitter.com/j09Hk25bcg
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#MWANANCHI Unaambiwa moja ya nne ya ubongo wa mwanadamu hutumika kulinda uimara wa macho, mtu anaona kwa msaada wa ubongo pic.twitter.com/RDRcU9QPl1
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#JamboLEO Wakazi waliobomolewa nyumba eneo la Magole A Kivule DSM wametoa simulizi za yaliyowakuta, ikiwemo kuombwa rushwa ili wasibomolewe pic.twitter.com/ponfWJbu4b
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
#JamboLEO Diamond akiri kuwa Bob Juniour ana mchango mkubwa kwenye maisha yake ya muziki lakini amesema hawezi kufanya naye kazi kwa sasa pic.twitter.com/matERfI8Hg
— millardayo (@millardayo) December 4, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA DECEMBER 4 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI