Ndani ya Heka Heka ya leo November 10, 2016 ipo na taarifa za mtoto mdogo aliyeibiwa na mfanyakazi wa ndani tangu mwaka 2003 akiwa na miaka miwili inadaiwa amepatikana huko wilayani Sengerema baada ya miaka 14 kupita.
Mtangazaji Geah Habibu amempata mama mzazi wa mtoto aliyepotea ambaye ameelezea tukio la kuibiwa kwa mtoto huyo lililotokea January 9, 2003 baada ya mfanyakazi wa ndani wa wifi kuondoka naye. Mama huyo anadai kuwa walifanya jitihada za kumtafuta sehemu nyingi bila mafanikio.
>>>”Alikuwa anaishi kwa shangazi yake, sasa kuna mama mmoja alikua anapita anatafuta kazi za ndani akapata kazi pale, kafanya kazi kwa mwezi mmoja na siku aliyopata mshahara wake akaondoka naye siku hiyo hiyo mida ya saa 1 jioni baada ya kumaliza kumuogesha akasema anaenda kununua kandambili akambeba mtoto ikawa ndio jumla.” – Mama Mtoto
Mama huyo amesema kuwa Jumamosi ya November 5 mwaka huu alipokea simu kutoka Mwanza kwa shemeji yake kwamba kuna mtoto amemuona na alipojaribu kumuangalia anamuona kafanana naye.
Baada ya kupata taarifa hizo mtoto alipelekwa Polisi ambako alihojiwa ili kujua sehemu waliko wazazi wake ambapo mtoto alijibu kuwa wako Sengerema ikabidi Askari, maafisa wa Ustawi wa Jamii pamoja na mama aliyepotelewa huyo mtoto waende Sengerema kuwaona wazazi wa huyo mtoto.
>>>”Baada ya kufika Sengerema tukaanzia Polisi wakasema wanaenda na ustawi wa jamii kwenda kijiji ambacho alioonekana mtoto, yaani yule mtoto nilivyomuona ni wa kwangu, hata nilivyomuona tu kwa mbali kiukweli hata mwili ulinisisimka sana. Mwanangu alikua na kovu ubavu wa kulia mgongoni ila kwasasa limeanza kufutika liko kwa mbali sana, tofauti na ilivyokuwa mwanzo.” – Mama Mtoto
Kusikiliza Full Stori, Bonyeza play hapa chini
VIDEO: MALALAMIKO YA WATEJA WA BENKI YA TWIGA KUHUSU KUPANGIWA HELA ZA KUTOA. VIDEO IKO HAPA CHINI